Tuesday, November 26, 2013

Wilson Masaka ndani ya Musoma akitokea Nairobits.

Mr.Maska akiwa na  Masister wa Baraki Sister's Farm akijaribu kuwapa mawaidha juu ya miradi yao waliyomwonesha na ikawa ni wakati sasa wa kumsikiliza kwa makini kabisa ushauri kutoka kwa Mr. masaka masaka .
Willison Masaka Training coordinator kutoka Nairobi kenya akitokea shirika la Nairobits School of Digital Design alifika Musoma Tanzania kuja kuhakikisha wanachuo wa Musoma Information Center wanakipata kile ambacho Wanachuo wa Nairobits wanachokipata pia kama ilivyokuwa makubaliano wakati wa kuanzisha chuo hiki cha Musoma Info. Center ambacho mpaka sasa ni tawi la chuo hicho cha nairobi na kile wanachuo wanachokisoma huko ndicho kinachofundishwa huku.

Ujio wa Mr. Masaka Musoma kiukweli ulikuwa ni mafanikio hasa kwa wanachuo na walimu pia kwa sababu Bwana Masaka ni mtu ambae anauzoefu wa kutosha wa mambo haya ya Design kwa sababu ni mtu ambae tangia chuo cha nairobits kinaanzishwa mnamo mwaka wa 2000 alikuwa ni mmoja wa manachuo waliofanikiwa kujiunga na chuo hatimae kuhitimu hapo na kutokana na uwezo wake wakawa wammepatia nafasi ya kuwa mwalimu hapo hapo na hajawahi kuwaangusha kwa kumpatia nafasi hiyo.

Hivyo basi uzoefu wake wa kazi alionao ulitosha kabisa kumpandisha cheo hadi kuwa "training coordinator" katika chuo hicho. Aliweza kufika musoma na kuja kuitizama Musoma Info. Center inaendeleaje pia hakuishia hapo bali alikuwa na kipindi na wanachuo kipindi chake kilikuwa kufundisha program moja ambayo ni muhimu sana kwa sasa ya "JOOMLA" wenyeji wa mambo haya hili si jina geni kwao kwa sababu ni muhimu sana kwa upande wetu sisi tunaojiita "developers" inatumika katika kuifanya tovuti iwe hai iweze kuonekana mtandaoni hivyo basi wanachuo walifurahi sana kuweza kuongeza  ujuzi mpya katika mafunzo yao.
                                    
 Hapa Ilifika wakati Bwana Masaka akajaribu kuwapima vijana hawa kama wana uwezo wa kuweza kuelezea kazi zao mbele ya kadamnasi basi kila mmoja wao alijaribu kumwonesha kuwa tayari uwezo amejengewa.
 Pamoja na kuwa tulipata ujuzi huo siyo hivyo tu pia baada ya mafunzo, tulipata muda wa kuweza kufuahia na Bwana Masaka uwanjani kwa sababu yeye ni mnazi wa mpira wa miguu hadi hapo alipo ameamua kuanzisha timu yake ijulikanayo kama "Mathare North Ranges"huko kwao ambayo yeye ndiyo kocha katika timu hiyo. Hapa pia tuliamua kufanya nae burudani ya pamoja kama unapoona katika picha.
                                    Baada ya Goli kupongezana lazima. Mimi Kushoto ( Mark Jay ) nikimpongeza Bwana Elly Munuve Kulia Baada ya kuifungia bao timu yetu. siku hiyo
Bwana Masaka Kushoto akiwa yuko hoi bada ya kuwa tumemkimbiza sana uwanjani huwezi amini kama Bwana Masaka na mwili wake ule angeweza kupiga chenga uwanjani na kufunga magoli mi mwenyewe nilikuwa siamini ila baada ya kushuhudia kweli niliamini kila kitu mazoezi tu ndilo jambo la msingi.

Victor Mandala mmoja wa timu ya Masaka akiwa anaufuatilia mpira uliopigwa mbele.
 Bwana Wilson Masaka akiwa na watu ambao maisha yao yote wamemtolea mungu sisi tunawaita masister. Wakiwa Musoma Maeneo ya kinesi huko ambako kuna kambi kubwa ya masiter hao wakiwa na makao yao makuu huko na wakiiendesha miradi yao huko.

Mradi baada ya Mradi tukimaliza kuangalia Ng'ombe twende tukaangalie ufugaji wa kuku, tukitoka hapo tuende tukaangalie dimbwi la samaki kisha nguruwe na miradi mingine ni mingi kiukweli unatembea hadi unachoka na maeneo yenyewe ni makubwa kiukweli wamewekeza vilivyo.