Tuesday, November 26, 2013

Baada ya Ujuzi Kazi

Baada ya Vijana hawa Musoma Information Center kupata ujuzi wa hapa na pale juu ya uundaji wa tovuti ( website ), sasa wameamua kuuonesha Uma kwamba wako tayari kusonga mbele, hizi hapa ni baadhi ya kazi zao za clients( wateja wao) ambazo wamewatengenezea kama majaribio ya kuwaonesha kuwa tayari wameiva na wako tayari kuanza maisha ya mapambano ya kujitegemea na si kutegemea wazazi tena.

Kiukweli ni kazi ngumu kuintengeneza tovuti( website) hadi ikamilike na iwekwe mtandaoni ni ni wachache wenye ujuzi huo hapa kwetu Tanzania, ukizingatia kuwa wahitaji wa tovuti hizo wakati mwingine inawalazimu kwenda nje ya nchi kutafuta wataalamu wa mambo hayo tena kwa gharama kubwa zaidi.

kutokana na shida Nairobits wakishirikiana na Terre des Hommes waliona ni vyema kuweza kuleta huduma hiyo karibu tena nchini tanzania kuweza kupunguza tatizo hilo hapa nchini na pia itakuwa imepunguza tatizo la vijana kukaa mtaani bila ajira ambalo ndilo suala kubwa ambalo limewatoa Terre des hommes kutoka uhoranzi kuja hapa tanzania. Kiukweli ni jambo la kuwashukuru kwa sababu wameleta mapinduzi makubwa hapa nchini hususani mkoa wa mara maana vijana wengi wameweza kubadilika kutoka mfumo hasi na kuingia mfumo chanya.

Nikisema mfumo hasi namaanisha mfumo ambao kijana tayari alikuwa amekata tamaa na maisha kutokana na matatizo yanayomsibu aidha kwa kuwapoteza wazazi wake au kutokana na hali ngumu ya maisha na kuwa mtumishi wa nyumbani ambaye tayari kaisha bebeshwa majukumu ya kifamilia kabla ya kupewa nyenzo za kupambania maishani.

Na pia ninapoongelea Mfumo Chanya ni mfumo  ambao kijana alikuwa ana ndoto maisha na hiyo ndo ikawa imeanza kufifia kwa namna fulani ghafla tena akapata msaada wa kuifanya ndoto yake iendelee kuwa hai na mwishoe kutimiza malengo yake.

Hizi hapa chini ni baadhi ya kazi ambazo vijana hao ambao ndoto zao zimefufuliwa wameweza kuzifanya kuudhibitishia uma kuwa wako tayari sasa kuanza maisha yao ya kujitegemea na si kutegemea tena.
GIVALEN MOTEL LTD.
Givalen Motel Ltd Ni Motel ambayo ina hadhi ya kimataifa ikiwa inapatikana Mkoani Mara wilaya ya Musoma wakiwa wanatoa huduma za kisasa kabisa. Wameona kuna umuhimu wa kuwa na tovuti na wakawa wameamua kumwamini mmoja kati ya wanachuo ajulikanae kama Annastella Gervase ambae ni Binti mdogo tu lakini machachali kabisa katika kazi hizi za design akiitumia vilivyo nafasi hii ya mwisho aliyoipata wazungu wanaiita "Golden chance" katika kuhakikisha kuwa hakuja musoma info. center kulala alikuja atoke anna mwingine ameamua kuwaonesha Givalen kuwa, kuwa mfupi si tatizo katika design amefanya kazi ambayo Givalen wenyewe hawakuweza kuamini kama kazi hii imefanyika hapahapa Tanzania.
Huu hapa ni ukurasa wa nje ya tovuti ya Givalen Motel Ltd kama ulivyotengenezwa na Annastella Gervase.

Unaposaidia ni sawa na umeweka akiba na siku zote "akiba haiozi" hayo ndo maneno ambayo mimi niyoweza kusema hapa kwenye ukurasa huu. hii haya ni tovuti ya "JIPE MOYO CENTER" Kituo ambacho kiukweli kama ni watu wenye moyo wa kusaidia kimejitolea kuwasidia vijana kujikomboa kimaisha. Kituo hiki kazi yake kubwa ni kuwakusanya watoto waliopo mtaani na kuwaleta katika kituo chao na kuanza kuwapatia mahitaji yao muhimu kama Elimu, Mavazi na Malazi kwa ujumla.

Ndiyo maana nikasema akiba haiozi nikimaanisha aliyewatengenezea tovuti hii ni kijana ambae wao wameweza kulea kuanzia akiwa mdogo hadi hapo alipofikia bado yupo mikononi mwao. hivyo basi waliweza kumleta katika chuo hiki cha musoma information center kama sehemu ya kuzidi kumwandalia maisha yake na hatimae hawajautia kumlea kijana huyu. namzungumzia BARAKA RICHARD ambae ndiye mtengenezaji wa tovuti hii unayoiona hapa na hakika JIPE MOYO kama lilivyo jina lao "JIPE MOYO MWISHO WA SIKU UTASHINDA" ndocho kilichotokea hapa.

Ukurasa wa nje ukionesha mazingira halisi ya kituo hiki na watoto ambao wanapata msaada wao kwa mjibu wa Baraka Richard.

SACCOS. shirika ambalo si geni kwa watanzania na ni shirika maarufu sana hapa Tanzania kutokana na huduma zake kuwa za wazi zaidi. Shirika ambalo linasaidia watu wengi wenye kipato cha chini pia wenye kipato cha juu katika kupata mikopo midogo midogo na mikubwa pia ili waweze kuanzisha biashara na miradi yao wenyewe. Shirika hili limekuwa nguzo nchini Tanzania katika kuwasaidia akina mama katika kuwapatia mikopo midogo midogo wakiwa katika vikundi ambavyo wao huvianzisha katika harakati za kujaribu kubadilisha maisha yao.

KIGERA SACCOS ni tawi lao ambalo lipo kigera wilaya ya musoma mkoa wa mara wakijaribu kuwafikishia wateja wake huduma kwa ukaribu zaidi huko vijijini maana waadhirika wakubwa wa tatizo hili wako vijijini kwa wingi hivyo basi SACCOS kama shirika la kukomboa maisha ya watu waliamua kuwasogezea huduma hukohuko walipo.

Hii hapa ni tovuti ambayo wametengenzewa na ELIZABETH JOSEPH mwanchuo wa Musoma Information Center. alipowatembelea na kuwapa ushauri juu ya umuhimu wa kuwa tovuti ya kuzitangaza huduma zao waliweza kuipata elimu hiyo kutoka kwa eliza na kuamua kumpa kandarasi hiyo na kama unavyoona hapo juu ni tovuti yao.
Kwa mjibu wa Elizabeth na Saccos wenyewe hiki ndicho walichotuletea.

MKOA WA MARA. ukitamka jina hili sehemu yoyote ile ukiwa nchini Tanzania hata mtoto ambae hana umri mkubwa sana anatambua moja kwa moja  unachotaka kikizungumzia. Ni mkoa ambao unatafsiriwa kwa matuko mbalimbali yakiwemo mauwaji, ujasiri wa kupindukia, mkoa ambao unatoa wanajeshi wa kutosha tena wa kujiamini ukitaja jeshi la Tanzania utakuwa unazungumzia mkoa wa mara. Swali ni kwa nini wanajeshi wengi wanatoka mkoa wa mara jibu ni mkoa ambao unatoa watu jasiri kabisa wanaofaa kuwa wanajeshi maana jeshi si sehemu ya kurudi nyuma kama ni twende wote twende si mwingine twende mwingine turudi. ni wapi unaweza kupata watu hao jibu mkoa wa mara.

Hii hapa ni tovuti iliyotengenezwa na kijana wa kike wa musoma information center ajulikanae kama SARAH LINKOLINI. Lengo la tovuti hii ni wewe kuweza kuujua kiundani zaidi mkoa wa mara. Hapa utapata kuujua mkoa wa mara vizuri kabisa na kwa undani zaidi wilaya zake, tamaduni zake, vyakula wanavyovipendelea wao kikiwemo "Kichuli" utaelewa kichuli ni nini, kabila zilizopo ndani ya mkoa huo na mwngineyo mengi hakika ukikose uhondo huu ni hapa hapa katika blog hii usiache kuitembelea usije ukakosa uhondo.
Hivi ndiyo maelezo yakavyokuwa yanatokea katika tovuti hii kipindi itakapokuwa mtandaoni.

Katika ulimwengu uliopita, wa sasa na ujao kama kuna mambo yataongelewa halafu fasheni isitajwe kiukweli hakuna atakaekuelewa unanazungumzia wakati gani. Fashion kama fasheni ni moja kati ya sehemu ambayo imetawala katika vichwa vya watu haijalishi ni wanawake, watoto wala wanaume kila kitu na fasheni si maneno yangu chukua muda angalia vitu vingi vinavyokuzunguka hapo ndipo utaweza kugundua ninachokizungumuza sijakurupuka ni kitu nimefanya uchunguzi ndo maana nikaja nacho hapao.
Huyu hapa ni mwanachuo wa Musoma Information Center  ukipenda muite "mama wa mashamsham" akiwa karibu nawe hata kama umenuna utafurahi tu maneno yake na lugha yake, jina lake halisi Shekha Khamisi ambaye yeye katika pitapita zake za kumtafuta mteja wake wa kumtengenezea tovuti yeye alimpata mtu ambaye yeye anahusika na uuzaji wa vitu mbalimbali vya vya fasheni kama unavyoona katika picha.anauza nguo mbalimabli, urembo mbalimbali na vinginevyo fika mwenyewe utajionea. si za kiume !!!, si za  Kike !!!! si za Watoto yaani hajabagua kiukweli zote zinapatikana kwa Mustafa fashion.