Tuesday, November 26, 2013


Wilson Masaka ndani ya Musoma akitokea Nairobits.

Mr.Maska akiwa na  Masister wa Baraki Sister's Farm akijaribu kuwapa mawaidha juu ya miradi yao waliyomwonesha na ikawa ni wakati sasa wa kumsikiliza kwa makini kabisa ushauri kutoka kwa Mr. masaka masaka .
Willison Masaka Training coordinator kutoka Nairobi kenya akitokea shirika la Nairobits School of Digital Design alifika Musoma Tanzania kuja kuhakikisha wanachuo wa Musoma Information Center wanakipata kile ambacho Wanachuo wa Nairobits wanachokipata pia kama ilivyokuwa makubaliano wakati wa kuanzisha chuo hiki cha Musoma Info. Center ambacho mpaka sasa ni tawi la chuo hicho cha nairobi na kile wanachuo wanachokisoma huko ndicho kinachofundishwa huku.

Ujio wa Mr. Masaka Musoma kiukweli ulikuwa ni mafanikio hasa kwa wanachuo na walimu pia kwa sababu Bwana Masaka ni mtu ambae anauzoefu wa kutosha wa mambo haya ya Design kwa sababu ni mtu ambae tangia chuo cha nairobits kinaanzishwa mnamo mwaka wa 2000 alikuwa ni mmoja wa manachuo waliofanikiwa kujiunga na chuo hatimae kuhitimu hapo na kutokana na uwezo wake wakawa wammepatia nafasi ya kuwa mwalimu hapo hapo na hajawahi kuwaangusha kwa kumpatia nafasi hiyo.

Hivyo basi uzoefu wake wa kazi alionao ulitosha kabisa kumpandisha cheo hadi kuwa "training coordinator" katika chuo hicho. Aliweza kufika musoma na kuja kuitizama Musoma Info. Center inaendeleaje pia hakuishia hapo bali alikuwa na kipindi na wanachuo kipindi chake kilikuwa kufundisha program moja ambayo ni muhimu sana kwa sasa ya "JOOMLA" wenyeji wa mambo haya hili si jina geni kwao kwa sababu ni muhimu sana kwa upande wetu sisi tunaojiita "developers" inatumika katika kuifanya tovuti iwe hai iweze kuonekana mtandaoni hivyo basi wanachuo walifurahi sana kuweza kuongeza  ujuzi mpya katika mafunzo yao.
                                    
 Hapa Ilifika wakati Bwana Masaka akajaribu kuwapima vijana hawa kama wana uwezo wa kuweza kuelezea kazi zao mbele ya kadamnasi basi kila mmoja wao alijaribu kumwonesha kuwa tayari uwezo amejengewa.
 Pamoja na kuwa tulipata ujuzi huo siyo hivyo tu pia baada ya mafunzo, tulipata muda wa kuweza kufuahia na Bwana Masaka uwanjani kwa sababu yeye ni mnazi wa mpira wa miguu hadi hapo alipo ameamua kuanzisha timu yake ijulikanayo kama "Mathare North Ranges"huko kwao ambayo yeye ndiyo kocha katika timu hiyo. Hapa pia tuliamua kufanya nae burudani ya pamoja kama unapoona katika picha.
                                    Baada ya Goli kupongezana lazima. Mimi Kushoto ( Mark Jay ) nikimpongeza Bwana Elly Munuve Kulia Baada ya kuifungia bao timu yetu. siku hiyo
Bwana Masaka Kushoto akiwa yuko hoi bada ya kuwa tumemkimbiza sana uwanjani huwezi amini kama Bwana Masaka na mwili wake ule angeweza kupiga chenga uwanjani na kufunga magoli mi mwenyewe nilikuwa siamini ila baada ya kushuhudia kweli niliamini kila kitu mazoezi tu ndilo jambo la msingi.

Victor Mandala mmoja wa timu ya Masaka akiwa anaufuatilia mpira uliopigwa mbele.
 Bwana Wilson Masaka akiwa na watu ambao maisha yao yote wamemtolea mungu sisi tunawaita masister. Wakiwa Musoma Maeneo ya kinesi huko ambako kuna kambi kubwa ya masiter hao wakiwa na makao yao makuu huko na wakiiendesha miradi yao huko.

Mradi baada ya Mradi tukimaliza kuangalia Ng'ombe twende tukaangalie ufugaji wa kuku, tukitoka hapo tuende tukaangalie dimbwi la samaki kisha nguruwe na miradi mingine ni mingi kiukweli unatembea hadi unachoka na maeneo yenyewe ni makubwa kiukweli wamewekeza vilivyo.

Baada ya Ujuzi Kazi

Baada ya Vijana hawa Musoma Information Center kupata ujuzi wa hapa na pale juu ya uundaji wa tovuti ( website ), sasa wameamua kuuonesha Uma kwamba wako tayari kusonga mbele, hizi hapa ni baadhi ya kazi zao za clients( wateja wao) ambazo wamewatengenezea kama majaribio ya kuwaonesha kuwa tayari wameiva na wako tayari kuanza maisha ya mapambano ya kujitegemea na si kutegemea wazazi tena.

Kiukweli ni kazi ngumu kuintengeneza tovuti( website) hadi ikamilike na iwekwe mtandaoni ni ni wachache wenye ujuzi huo hapa kwetu Tanzania, ukizingatia kuwa wahitaji wa tovuti hizo wakati mwingine inawalazimu kwenda nje ya nchi kutafuta wataalamu wa mambo hayo tena kwa gharama kubwa zaidi.

kutokana na shida Nairobits wakishirikiana na Terre des Hommes waliona ni vyema kuweza kuleta huduma hiyo karibu tena nchini tanzania kuweza kupunguza tatizo hilo hapa nchini na pia itakuwa imepunguza tatizo la vijana kukaa mtaani bila ajira ambalo ndilo suala kubwa ambalo limewatoa Terre des hommes kutoka uhoranzi kuja hapa tanzania. Kiukweli ni jambo la kuwashukuru kwa sababu wameleta mapinduzi makubwa hapa nchini hususani mkoa wa mara maana vijana wengi wameweza kubadilika kutoka mfumo hasi na kuingia mfumo chanya.

Nikisema mfumo hasi namaanisha mfumo ambao kijana tayari alikuwa amekata tamaa na maisha kutokana na matatizo yanayomsibu aidha kwa kuwapoteza wazazi wake au kutokana na hali ngumu ya maisha na kuwa mtumishi wa nyumbani ambaye tayari kaisha bebeshwa majukumu ya kifamilia kabla ya kupewa nyenzo za kupambania maishani.

Na pia ninapoongelea Mfumo Chanya ni mfumo  ambao kijana alikuwa ana ndoto maisha na hiyo ndo ikawa imeanza kufifia kwa namna fulani ghafla tena akapata msaada wa kuifanya ndoto yake iendelee kuwa hai na mwishoe kutimiza malengo yake.

Hizi hapa chini ni baadhi ya kazi ambazo vijana hao ambao ndoto zao zimefufuliwa wameweza kuzifanya kuudhibitishia uma kuwa wako tayari sasa kuanza maisha yao ya kujitegemea na si kutegemea tena.
GIVALEN MOTEL LTD.
Givalen Motel Ltd Ni Motel ambayo ina hadhi ya kimataifa ikiwa inapatikana Mkoani Mara wilaya ya Musoma wakiwa wanatoa huduma za kisasa kabisa. Wameona kuna umuhimu wa kuwa na tovuti na wakawa wameamua kumwamini mmoja kati ya wanachuo ajulikanae kama Annastella Gervase ambae ni Binti mdogo tu lakini machachali kabisa katika kazi hizi za design akiitumia vilivyo nafasi hii ya mwisho aliyoipata wazungu wanaiita "Golden chance" katika kuhakikisha kuwa hakuja musoma info. center kulala alikuja atoke anna mwingine ameamua kuwaonesha Givalen kuwa, kuwa mfupi si tatizo katika design amefanya kazi ambayo Givalen wenyewe hawakuweza kuamini kama kazi hii imefanyika hapahapa Tanzania.
Huu hapa ni ukurasa wa nje ya tovuti ya Givalen Motel Ltd kama ulivyotengenezwa na Annastella Gervase.

Unaposaidia ni sawa na umeweka akiba na siku zote "akiba haiozi" hayo ndo maneno ambayo mimi niyoweza kusema hapa kwenye ukurasa huu. hii haya ni tovuti ya "JIPE MOYO CENTER" Kituo ambacho kiukweli kama ni watu wenye moyo wa kusaidia kimejitolea kuwasidia vijana kujikomboa kimaisha. Kituo hiki kazi yake kubwa ni kuwakusanya watoto waliopo mtaani na kuwaleta katika kituo chao na kuanza kuwapatia mahitaji yao muhimu kama Elimu, Mavazi na Malazi kwa ujumla.

Ndiyo maana nikasema akiba haiozi nikimaanisha aliyewatengenezea tovuti hii ni kijana ambae wao wameweza kulea kuanzia akiwa mdogo hadi hapo alipofikia bado yupo mikononi mwao. hivyo basi waliweza kumleta katika chuo hiki cha musoma information center kama sehemu ya kuzidi kumwandalia maisha yake na hatimae hawajautia kumlea kijana huyu. namzungumzia BARAKA RICHARD ambae ndiye mtengenezaji wa tovuti hii unayoiona hapa na hakika JIPE MOYO kama lilivyo jina lao "JIPE MOYO MWISHO WA SIKU UTASHINDA" ndocho kilichotokea hapa.

Ukurasa wa nje ukionesha mazingira halisi ya kituo hiki na watoto ambao wanapata msaada wao kwa mjibu wa Baraka Richard.

SACCOS. shirika ambalo si geni kwa watanzania na ni shirika maarufu sana hapa Tanzania kutokana na huduma zake kuwa za wazi zaidi. Shirika ambalo linasaidia watu wengi wenye kipato cha chini pia wenye kipato cha juu katika kupata mikopo midogo midogo na mikubwa pia ili waweze kuanzisha biashara na miradi yao wenyewe. Shirika hili limekuwa nguzo nchini Tanzania katika kuwasaidia akina mama katika kuwapatia mikopo midogo midogo wakiwa katika vikundi ambavyo wao huvianzisha katika harakati za kujaribu kubadilisha maisha yao.

KIGERA SACCOS ni tawi lao ambalo lipo kigera wilaya ya musoma mkoa wa mara wakijaribu kuwafikishia wateja wake huduma kwa ukaribu zaidi huko vijijini maana waadhirika wakubwa wa tatizo hili wako vijijini kwa wingi hivyo basi SACCOS kama shirika la kukomboa maisha ya watu waliamua kuwasogezea huduma hukohuko walipo.

Hii hapa ni tovuti ambayo wametengenzewa na ELIZABETH JOSEPH mwanchuo wa Musoma Information Center. alipowatembelea na kuwapa ushauri juu ya umuhimu wa kuwa tovuti ya kuzitangaza huduma zao waliweza kuipata elimu hiyo kutoka kwa eliza na kuamua kumpa kandarasi hiyo na kama unavyoona hapo juu ni tovuti yao.
Kwa mjibu wa Elizabeth na Saccos wenyewe hiki ndicho walichotuletea.

MKOA WA MARA. ukitamka jina hili sehemu yoyote ile ukiwa nchini Tanzania hata mtoto ambae hana umri mkubwa sana anatambua moja kwa moja  unachotaka kikizungumzia. Ni mkoa ambao unatafsiriwa kwa matuko mbalimbali yakiwemo mauwaji, ujasiri wa kupindukia, mkoa ambao unatoa wanajeshi wa kutosha tena wa kujiamini ukitaja jeshi la Tanzania utakuwa unazungumzia mkoa wa mara. Swali ni kwa nini wanajeshi wengi wanatoka mkoa wa mara jibu ni mkoa ambao unatoa watu jasiri kabisa wanaofaa kuwa wanajeshi maana jeshi si sehemu ya kurudi nyuma kama ni twende wote twende si mwingine twende mwingine turudi. ni wapi unaweza kupata watu hao jibu mkoa wa mara.

Hii hapa ni tovuti iliyotengenezwa na kijana wa kike wa musoma information center ajulikanae kama SARAH LINKOLINI. Lengo la tovuti hii ni wewe kuweza kuujua kiundani zaidi mkoa wa mara. Hapa utapata kuujua mkoa wa mara vizuri kabisa na kwa undani zaidi wilaya zake, tamaduni zake, vyakula wanavyovipendelea wao kikiwemo "Kichuli" utaelewa kichuli ni nini, kabila zilizopo ndani ya mkoa huo na mwngineyo mengi hakika ukikose uhondo huu ni hapa hapa katika blog hii usiache kuitembelea usije ukakosa uhondo.
Hivi ndiyo maelezo yakavyokuwa yanatokea katika tovuti hii kipindi itakapokuwa mtandaoni.

Katika ulimwengu uliopita, wa sasa na ujao kama kuna mambo yataongelewa halafu fasheni isitajwe kiukweli hakuna atakaekuelewa unanazungumzia wakati gani. Fashion kama fasheni ni moja kati ya sehemu ambayo imetawala katika vichwa vya watu haijalishi ni wanawake, watoto wala wanaume kila kitu na fasheni si maneno yangu chukua muda angalia vitu vingi vinavyokuzunguka hapo ndipo utaweza kugundua ninachokizungumuza sijakurupuka ni kitu nimefanya uchunguzi ndo maana nikaja nacho hapao.
Huyu hapa ni mwanachuo wa Musoma Information Center  ukipenda muite "mama wa mashamsham" akiwa karibu nawe hata kama umenuna utafurahi tu maneno yake na lugha yake, jina lake halisi Shekha Khamisi ambaye yeye katika pitapita zake za kumtafuta mteja wake wa kumtengenezea tovuti yeye alimpata mtu ambaye yeye anahusika na uuzaji wa vitu mbalimbali vya vya fasheni kama unavyoona katika picha.anauza nguo mbalimabli, urembo mbalimbali na vinginevyo fika mwenyewe utajionea. si za kiume !!!, si za  Kike !!!! si za Watoto yaani hajabagua kiukweli zote zinapatikana kwa Mustafa fashion.

James Maina Atua Musoma Information Center Kuleta kitu kipya

James Maina Kutoka Nairobi kenya akiwa ni Mwalimu mzoefu wa mambo ya Design akitokea katika shirika la Nairobits School of Digital Design( www.nairobits.com).Alipewa nafasi ya kuweza kuwatembelea wanafunzi wa Musoma Information Center ambacho ni chuo kinachofundisha mambo ya webdesign and Programming kwa lugha ya kitaalam kuweza kuwaletea kitu kigeni katika mafunzo yao. Alikuja Musoma kwa ajili ya kuwafundisha vijana kitu kigeni kinaitwa "Information Architecture". na "Design/Creative thinking".

Kiukweli hapa vijana walipata nafasi ya kuweza kujifunza mambo muhimu sana ambayo wanatakiwa kuyafanya wanapokuwa wamewapata wateja wao wa kumtengenezea tovutu ( website)
Vijana walipata kujua ni jinsi gani anaweza kuongea na mteja wake na pia walipewa mwanga juu ya vitu ambavyo mteja wake anafaa kumpatia ili aweze kumtengenezea tovuti.
Pia walielekezwa jinsi gani wao kama web designer wanaweza kukaa chini na kupangilia mfumo mzima wa tovuti itakavyokaa na kuendana na hitaji la mteja wake.

JAMES MAINA akiwa katika maandalizi ya kipindi maana hakuna jambo zuri ambalo litafanyika bila maandalizi
Wanachuo wa Musoma Information Center walipomapata ujuzi huo kutoka kwa bwana James Maina ilifikia wakati wa kuanza kufanya kwa vitendo na kama unavyoona katika picha hawa ni baadhi ya wanachuo wakiwa katika zoezi la kuonesha ni nini wamejifunza kutoka kwa Bwana James.
Mmoja kati ya wanachuo waliopata mafunzo hayo akijulikana kama " Uyanjo Yakobo" akijaribu kuweka maelekezo aliyoyapata katika karatasi hatimae ayahamishie katika computer.

Ushirikiano katika kusoma ni jambo la kujenga sana, kwa sababu ukileta nilichokipata na mimi nikaleta changu tunakuwa na kitu kizima tuliokanyaga umande tunalitambua hilo.
Baada ya majadiliano twende kazi sasa kutoka kushoto Janepha Nassoro, Victor Mandara na Shekha Khamisi wakiwa katika harakati za kutaka kumwonesha Bwana James Maina kuwa safari yake kutoka Nairobi Kenya Hadi Musoma Tanzania haijaenda bure kuna kitu kweli kaleta.