Kiukweli hapa vijana walipata nafasi ya kuweza kujifunza mambo muhimu sana ambayo wanatakiwa kuyafanya wanapokuwa wamewapata wateja wao wa kumtengenezea tovutu ( website)
Vijana walipata kujua ni jinsi gani anaweza kuongea na mteja wake na pia walipewa mwanga juu ya vitu ambavyo mteja wake anafaa kumpatia ili aweze kumtengenezea tovuti.
Pia walielekezwa jinsi gani wao kama web designer wanaweza kukaa chini na kupangilia mfumo mzima wa tovuti itakavyokaa na kuendana na hitaji la mteja wake.
![]() |
| JAMES MAINA akiwa katika maandalizi ya kipindi maana hakuna jambo zuri ambalo litafanyika bila maandalizi |
![]() |
| Mmoja kati ya wanachuo waliopata mafunzo hayo akijulikana kama " Uyanjo Yakobo" akijaribu kuweka maelekezo aliyoyapata katika karatasi hatimae ayahamishie katika computer. |
![]() |
| Ushirikiano katika kusoma ni jambo la kujenga sana, kwa sababu ukileta nilichokipata na mimi nikaleta changu tunakuwa na kitu kizima tuliokanyaga umande tunalitambua hilo. |
































